Tuesday, 18 March 2014

maadhimisho ya siku ya pai duniani

Maadhimisho ya Siku ya Pai, Matukio

 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani na wanafunzi wa Shule ya Msingi Lumumba wakiandamana wakati wa maadhimisho ya siku ya PAI (PI) Duniani jijini Dar es Salaam.


 Wanafunzi wa Shule za Msingi za Dar es Salaam za Uhuru Wasichana, Uhuru Mchanganyiko Lumumba na baadhi ya Shule za Sekondari wakiandamana kuadhimisha siku ya Pai (PI) duniani iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam.

 Haya sasa nyimbo zinaponogeshwa utanijua mieeeeeee.


 Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa Kassim Majaliwa(kushoto) akiangalia vitabu kwenye maonyesho ya vitabu yaliyoambatana na maadhimisho ya Siku ya Pai duniani jijini Dar es Saalaam, kulia ni wafanyakazi wa Taasisi ya kusaidia Elimu ya Pearson Meneja wa Mauzo/ Masoko Catherine Fred na Muhasibu Nabil Karatela wakimpa maelezo.


 Mhasibu wa Pearson (wadau wa elimu) Nabill Karatela akigawa kalenda kwa wanafunzi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya PI.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani Haman Mohamed (kulia) na Lilian Tesha wakiangalia vitabu wakati wa maonyesho yaliyofanyika shuleni hapo ambayo yaliambatana sambamba na maadhimisho ya Siku ya Pai (PI) duniani.

No comments:

Post a Comment