Maadhimisho ya Siku ya Pai, Matukio
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani na wanafunzi wa Shule ya
Msingi Lumumba wakiandamana wakati wa maadhimisho ya siku ya PAI (PI)
Duniani jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule za Msingi za Dar es Salaam za Uhuru Wasichana, Uhuru
Mchanganyiko Lumumba na baadhi ya Shule za Sekondari wakiandamana
kuadhimisha siku ya Pai (PI) duniani iliyoadhimishwa jijini Dar es
Salaam.
Haya sasa nyimbo zinaponogeshwa utanijua mieeeeeee.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa na Serikali
za Mitaa Kassim Majaliwa(kushoto) akiangalia vitabu kwenye maonyesho ya
vitabu yaliyoambatana na maadhimisho ya Siku ya Pai duniani jijini Dar
es Saalaam, kulia ni wafanyakazi wa Taasisi ya kusaidia Elimu ya Pearson
Meneja wa Mauzo/ Masoko Catherine Fred na Muhasibu Nabil Karatela
wakimpa maelezo.
Mhasibu wa Pearson (wadau wa elimu) Nabill Karatela akigawa kalenda kwa
wanafunzi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya PI.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani Haman Mohamed (kulia) na
Lilian Tesha wakiangalia vitabu wakati wa maonyesho yaliyofanyika
shuleni hapo ambayo yaliambatana sambamba na maadhimisho ya Siku ya Pai
(PI) duniani.